Kongamano la 7 la Biashara na Uwekezaji baina ya Israel na Tanzania, ambalo linaitwa Tanzania Israel Business and Investment Forum (TIBIF) linatarajia kufanyika tarehe 16 - 24 mwezi wa kumi 2023, huko Tel Aviv Israel, Kongamano la mwaka huu ni la 7 tangu kuanza kufanyika, na litafanyika kwa pamoja na kongamano kuu la 21 la kilimo Duniani kwa jina la AGRITECH.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni: Usalama wa Chakula katika kipindi cha Changamoto za Kidunia: Kuwezesha ubunifu duniani wa sekta za Kilimo, Chakula na Maji.
Kongamano la 7 la TIBIF linaratibiwa kwa pamoja na Taasisi za Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT), (AGRITECH-Israel) na Israel Africa Chamber of Commerce, kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Israel kupitia Wizara zake za Mambo ya Nje, Wizara ya Kilimo, Taasisi ya Usafirishaji na Ushirikiano wa Kimataifa ya Israeli (IEICI), na Wizara ya Uchumi, uwekazaji na Viwanda pamoja na taasisi zingine za sekta binafsi na kilimo. Kongamano hili linakuja baada ya makongamano sita ya awali yaliyokuwa na mafanikio makubwa yakifanyika kwa pamoja katika majiji ya Dar es Salaam, Tanzania na Tel Aviv, Israel.
Kongamano la mwaka huu litawaleta pamoja wawekezaji, wafanyabiashara mashuhuri, wajasiriamali, maofisa wa Serikali, na Wakurugenzi Wakuu wa sekta binafsi kutoka pande zote mbili kwa ajili ya kuendeleza ubunifu, biashara na uhusiano baina ya nchi hizo mbili ambayo yalikita mizizi kutoka kwenye makongamano yaliyopita.Kwa upande wa viongozi wa juu kiserikali wamealikwa mawaziri mbalimbali pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Kilimo, mifugo na uvuvi, Viwanda na Biashara, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Maji na utalii.
Lengo kuu la kongamano hili ni kutoa fursa sawa kwa nchi zote mbili kunufaika na uhusiano wa kibiashara na miradi, na litapambwa na maonyesho, pamoja na matembezi ya kitaaluma ya vitendo kwenye sekta husika.
kama unachangamoto ya kifedha
tunazo bank washirika ambazo ni Equity Bank pamoja na Maendeleo Bank wao wanatoa mkopo wa safari kwa namna rahisi sana ili kila mmoja aweze kujiunga na safari hii
Tafadhali! tembelea tovuti ya www.tibif.klnt.org , au simu 0752 715 098.
Welcome to the Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) is a network of leaders in ministry, church, and business, government, politics, other professional circles and intercessors who are united in their passion to advance the kingdom of God in Tanzania.